BREAKING: PRINCE Dube mshambuliaji namba moja ndani ya Ligi Kuu Bara leo Novemba 9 ametangazwa kuwa mchezaji Bora wa Mwezi Septemba.
Kwa mwezi Septemba, Dube alifunga mabao manne na kutoa pasi moja ya bao.
Dube ndani ya Ligi Kuu Bara ametupia jumla ya mabao matano na pasi mbili za mabao.
Nyota huyo amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) msimu wa 2020/21 baada ya kuwashinda wenzake alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar na Kamati ya Tuzo ya VPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali, ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu.
Septemba kila timu ilicheza michezo minne na Dube alionesha kiwango kikubwa na kuiwezesha Azam kushinda michezo yote, hivyo kupata pointi 12 na kuongoza ligi ambapo Dube alifunga mabao matatu na kutoa pasi moja iliyozaa bao.
Azam ilizifunga Polisi Tanzania FC 1-0, Coastal Union FC 2-0, Mbeya City FC 0-1 na Tanzania Prisons FC 0-1.
Dube aliwashinda kipa wa Azam, David Kissu na kiungo wa Simba SC, Clatous Chama aliyetupia mabao mawili na pasi mbili za mabao ambapo Kissu aliiongoza Azam kushinda katika michezo yote bila ya kuruhusu bao, hivyo timu hiyo kuongoza ligi.
Anastahiki na hata hii october atatwaa yy tna mana gemu yamwanzo ya mwezi huu ana goli mbili na assist moja, wengine mara hii watasubir kwanza kdgo.
ReplyDelete