October 9, 2020

 


BREAKING: Aristica Cioaba, Kocha Mkuu wa Klabu ya Azam FC ametangazwa kuwa kocha bora kwa mwezi Septemba.

Leo Oktoba 9, Cioaba raia wa Romania ametangazwa kutwaa tuzo hiyo.

Cioaba ambaye kwenye mechi nne za mwezi Septemba alishinda zote na timu yake haikufungwa bao aliwashinda makocha wawili ambao ni Sven Vandenbroeck wa Simba na Zlatko Krmpotic wa Yanga.


Cioaba alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar wiki hii na Kamati ya Tuzo ya VPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu.

Cioaba alishinda michezo yote minne wakati Sven na Zlatco kila mmoja alishinda michezo mitatu na kutoka sare mmoja.

Sven aliiongoza Simba kuifunga Ihefu SC 0-1, Biashara United FC 4-0, Gwambina FC 3-0 na ilitoka sare ugenini na Mtibwa Sugar FC 1-1, Uwanja wa Jamhuri wakati Zlatco alishinda dhidi ya Mbeya City FC 1-0, Kagera Sugar FC 0-1 na Mtibwa Sugar FC 0-1 na alitoka sare na Prisons FC 1-1, Uwanja wa Mkapa.

 Simba ilimaliza mwezi Septemba ikiwa ya pili na Yanga ilikuwa ya tatu zikitofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.


Simba ilifunga mabao 10 na Yanga ilifunga mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara.

5 COMMENTS:

  1. Atawaburuza Mpaka mwisho wa Msimu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Azam FC atachukua Ubingwa....Chamazi wana jambo Lao mwaka huu

      Delete
    2. Sawa utopolo tumewasikia mmehama kushabikia timu yenu

      Delete
    3. Uwezo huo Azam Hana, Azam muda cmrefu atakuwa na kmc

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic