MANCHESTER United imekubali kupata saini ya mshambuliaji wa PSG, Edinson Cavan kwa dili la miaka miwili akiwa ni mchezaji huru.
Ripoti zinaeleza kuwa mazungumzo ya haraka yalianza kufanyika jana Oktoba 3 ikiwa ni muda mfupi kabla ya dirisha la usajili kufungwa Oktoba 5 na inaripotiwa kuwa raia huyo wa Uruguay leo amefanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini dili lake jipya.
Cavani mwenye miaka 33 huenda akatangazwa rasmi kuwa mali ya Manchester United kesho, Oktoba 5 kwa mashabiki wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu England.
Cavan ambaye aliibukia ndani ya PSG akitokea Klabu ya Napoli msimu wa 2013, mpaka msimu wa 2020 alikuwa amecheza jumla ya michezo 200 na kutupia kimiani mabao 138.
0 COMMENTS:
Post a Comment