October 8, 2020

 


KIKOSI cha KMC ‘Wana Kino Boys’ kimezidi kuwa na majanga ndani ya dakika 180 baada ya kushindwa kufunga bao kwenye mechi zake mbili mfululizo ikipoteza ile kasi iliyoanza nayo mwanzo.

 

Oktoba 5, Uwanja wa Uhuru, KMC ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania baada ya kutoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 ilipomenyana na Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba, Septemba 25.

 

Bao la ushindi kwa Polisi Tanzania lilifungwa na Pius Buswita baada ya kutokea piga nikupige ndani ya lango la KMC lililokuwa chini ya nahodha Juma Kaseja aliyeokota mpira nyavuni dakika ya 88.


Kwenye mechi zake tatu za mwanzo, safu ya ushambuliaji ya KMC ilifunga mabao nane na safu ya ulinzi iliruhusu mabao mawili na KMC iliweza kuongoza ligi kwenye raundi tatu ila kwa sasa ipo nafasi ya saba na pointi tisa ikiwa imefungwa jumla ya mabao manne.

 

Buswita, mfungaji wa bao la Polisi Tanzania ameliambia Championi Jumatano kuwa, ushirikiano ndani ya kikosi uliwapa nguvu ya kushinda.


Kwa upande wa KMC kiongozi wa benchi la ufundi, John Simkoko alisema kuwa adhabu aliyopata kocha Habib Kondo baada ya timu yake kupata matatizo ilipocheza na Kagera Sugar ilikuwa ni sababu ya kupoteza kwa kuwa alifungiwa mechi tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic