UONGOZI wa Yanga umesema kuwa ulikuwa unawatamani wapinzani wao Simba kukutana nao Oktoba 18 kwa kuwa hawakuwa na ujanja lazima wangeshinda kutokana na kikosi chao kuwa kwenye mwendo mzuri.
Awali ilipaswa mchezo huo wa Yanga na Simba kuchezwa Oktoba 18, Uwanja wa Mkapa ila taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania, Oktoba 7 ilieleza kuwa mchezo huo umefanyiwa mabadailiko na utachezwa Novemba 7.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa walikuwa na shauku kubwa ya kucheza na Simba mwezi huu ili wawape kile ambacho wanastahili.
"Nakwambia tena hakika ilikuwa ni lazima tuwapige pale kwa Mkapa na tulikuwa tunawatamani kwelikweli tukutane nao uwanjani, bahati yao tumewakosa mwezi Oktoba.
"Unajua kwa namna ambavyo kikosi chetu kilikuwa kinakwenda na namna ambavyo wachezaji wetu ni bora basi hawakuwa na ujanja wapinzani wetu walikuwa wanachapwa mapema tu ndani ya uwanja.
"Ukitazama mwendo wetu na wao hatukua tofauti katika matokeo zaidi wametuzidi idadi ya mabao ya kufunga sasa hapo unadhani tofauti ipo wapi? Hakuna kwa kuwa tarehe imepelekwa mbele basi tunawasubiri hiyo Novemba 7.
"Kwa sasa tunaendelea na maandalizi ya mechi nyingine kwani kuna mechi nyingi za kucheza sio lazima iwe hao watani ila ni lazima tutafanya kweli," amesema.
Kesho Yanga itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC, Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:00 usiku.
Kwenye msimamo wa ligi zote zikiwa zimecheza mechi tano, Simba ipo nafasi ya pili ikiwa imefunga mabao 14 huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu imefunga mabao 7.
Zote zina pointi 13 kwa kuwa zimeshinda mechi nne na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mechi zao.
Simba ilitoka sare na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Yanga ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa.
hata mechi iliyopita ya Simba na Yanga alisema hivyo.Hivi anajua hadi sasa Simba ina jumla ya mabao mara mbili ya Yanga..Kocha aliyekuja alitambulishwa kwa mbwembwe wakati ukweli uko wazi. Kaze alifanya kazi Bacerona...na ukiacha timu alizifundisha Rwanda na Burundi zingine zote huko Canada anafundisha U20.Ukweli kupata zile goli moja moja ni bahati..Na Coastal walipoteana kipindi cha pili kama Yanga walivyopoteana siku anapigwa 4G.Kama umesahau na mechi iliyopita ulisema hivyo.
ReplyDeleteTambua anakuja kocha mpya bado atahitaji kuitambua timu na kuizoea.November 7 ni pafupi sana
Tatizo we mkia hujui soka na utabaki kukalili tuu,siku mmempiga jangwani wachezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza wote walikuwa majeruhi na mwingine mkamuhonga ili acheze vibaya mumchukue. Kisoka Yanga inaskauti makini kiusajiri wakat mikia ndio wale mnaoingia kwenye mtihani na kucopy mpaka jina la mwenzio. Sikuhizi sio analogy kila kitu kipo mtandaoni,muda wa 5G unakaribia wakimataifa just wait time will tell
DeleteYanga kweli kichwa ngumu. Wangeifunga simba kwa timu gani waliyonayo? Au walikuwa wamemaliza mitego na wachawi wao? Wahamishe tuu hiyo mizinga tar 7 bado kuna muda na hivi kocha aliyekataa mbo ya ulozi kaondolewa sasa full gamboshi. Ha ha ha
ReplyDeleteJe wewe uchawi ulishaacha kk na tokea umeanza kuloga umepata faida gani mbona tunacheza wote chandimu humuhumu ukitoka tu unakula mkono au umesahau kk
ReplyDeleteUkweli ni kwamba Yanga ya sasaiv inawachezaji wenye uwezo wengi, uwezi kufananisha na msimu uliyopita,labda Kama una akili za mgando
ReplyDeleteHumu humumu tumemkariri Antony Nugaz akichekelea kusogezwa kwa mchezo akisema wamepata nafasi ya kuandaa kikosi chao vizuri.Someni hiyo taarifa iko humu,hii kauli nyingine.Kumbuka hiki kikosi cha yanga kina wachezaji wengi wangi,muunganiko wa wachezaji ndio unaanza kukakaa vizuri,muda ulikuwa unahitajika kuweka mambo sawa,kumbukeni kocha mkuu bado mgeni baada ya timua timua kwann yanga wasishukuru mechi kusogezwa mbele?
ReplyDeleteNugaz haeleweki coz yy ndo alitoa taarifa ya kufurahia kuahirishwa kwa mechi leo anasema tulitamani kukutana na simba oct 18, tuelewe nini hapa?
ReplyDelete