BAADA ya kufanikiwa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Septemba ndani ya Ligi Kuu Bara, straika wa Azam FC, Prince Dube, amebainisha kwamba anataka kuwa bora zaidi ndani ya kikosi hicho.
Dube raia wa Zimbabwe, ameongeza kwamba anataka kuwa bora zaidi na kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika mechi zake za ligi na michuano mingine msimu huu.
Mzimbabwe huyo alitwaa tuzo hiyo baada ya kuhusika katika mabao manne ambapo alifunga matatu na asisti moja kwa mwezi Septemba.
Dube ameliambia Spoti Xtra kuwa: “Nawashukuru wachezaji wenzangu pamoja na makocha kwa tuzo hii. Hii siyo kwa ajili yangu pekee bali kwa timu nzima, ninafurahia mchango wa kila mtu.
“Nataka kuwa bora zaidi kwa timu, tushinde mechi zetu kama timu na pia tuendelee kufanya vizuri zaidi katika mechi zinazokuja.”
0 COMMENTS:
Post a Comment