CHRISTINA Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa baada ya timu hiyo kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania hasira zao ni kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union.
Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Uhuru, Oktoba 14 unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa timu zote zimetoka kupoteza pointi tatu kwenye mechi zao tatu zilizopita.
KMC Oktoba 5 ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Uhuru na Coastal Union ilifungwa mabao 3-0 dhidi ya Yanga, Oktoba 3.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina amesema kuwa makosa waliyoyafanya kwenye mechi zao mbili zilizopita wameyaona na watayafanyia kazi.
“Tulipoteza mchezo wetu wa kwanza uwanja wa nyumbani haina maana kwamba tutaendelea kupoteza hapana bado tuna mechi nyingi na tutaanza na Coastal Union Uwanja wa Uhuru Jumatano tunaamini tutafanya kweli.
"Maandalizi yapo sawa na kila kitu kipo vizuri kikubwa mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kuona burudani burudani ndani ya uwanja," amesema.
KMC ipo 7 ikiwa na pointi 9 inakutana na Coastal Union iliyo nafasi ya 15 na pointi 4.
0 COMMENTS:
Post a Comment