October 8, 2020

 


Na Saleh Ally

Nilikuwa naangalia mechi za nusu fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika pia Kombe la Shirikisho, kama ni mgumu wa kutafakari inaumiza sana, ntakuambia kwa nini.

Nasema inaumiza ukianza na Ligi ya Mabingwa Afrika, timu nne zilizo nusu fainali, utagundua zote zinatoka Afrika Kaskazini katika nchi mbili za Misri na Morocco.

Nusu Fainali ya Kwanza:- Waydad (Morocco) Vs Al Ahly (Misri).

Nusu Fainali ya Pili:- Raja (Morocco) Vs Zamalek (Misri)

Upande wa Kombe la Shirikisho
Nusu Fainali ya Kwanza: RS Berkane (Morocco) Vs Hausa (Morocco).

Nusu Fainali ya pili: Pyramids (Misri) Vs Horoya (Guinea).

Utagundua katika timu nane hatua ya nusu fainali kwa maana ya timu nne za ligi ya mabingwa na nne za kombe la shirikisho, ni moja tu inatokea Afrika Magharibi na zile za Afrika Kaskazini kwa maana ya timu saba zilizobaki zinatokea katika nchi mbili tu.

Misri wakiwa wameingiza timu zao vigogo katika Ligi ya Mabingwa na moja katika Kombe la Shirkisho lakini Morocco unaona wametawala katika Kombe la Shirikisho wakiwa na timu moja katika Ligi ya Mabingwa.

Katika hali ya kawaida lazima ujiulize, tuko wapi sisi. au kwanini hatupo hapa na itaendelea kuwa hivi hadi lini? Kuna jambo la kujiuliza na lazima tufikirie kwamba bado kuna shida sehemu na hatufikirii kama tunaweza kufika huko maana mawazo yetu ni Simba na Yanga na matusi tu.

Mawazo yetu ni chuki, mawazo yetu ni watu kusema uongo na vitu wasivyovijua kwa maana ya kukamata uzushi na kuufanya ukweli bila ya kuwa na uhakika.

 Chuki ya rangi, chuki za kipuuzi ambazo zinatufanya mawazo yetu yabakie hapa nyumbani tukishindana kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Mapinduzi.

Jiulizeni, kwani Morocco au Misri hawana ushindani wa timu zao kubwa? Sote tunajua ushindani wao uko juu zaidi yetu. Lakini vipi wapo hapo kimafanikio? Watu wanajua kuutumia mpira kama burudani na biashara kubwa.

 Mipango ya viongozi si ya juujuu na watu wanashindana maendeleo. Hapa tunashindana kumgombea Morrison na propaganda lukuki.

Viongozi badala ya kuamini kazi yao kubwa ni KULETA MAENDELEO, wao wanaamini mafanikio ni KUPENDWA NA MASHABIKI.

Lazima mbadilike ili kuwabadilisha wengine na mpira wenyewe.

4 COMMENTS:

  1. Ninyi waandishi wa habari hasa wewe mnachangio propaganda za mpira wa miguu Tanzania

    ReplyDelete
  2. Tena we Sareh jembe we ndo kalai kabisa, unaandika vitu bila kuwa na uhakika kwahiyo watu kama nyie ni ovyo kabisa na mnarudisha nyuma mpira wetu kwa kuandika taarifa za uongo na za ninafika yani , tena we una usimba mwingi mbumbumbu we

    ReplyDelete
  3. Unakumbuka yanga walivyofurahia simba kutolewa raundi ya kwanza champion league? Hivi sasa simba wanashiriki champion league Yanga wanaishia kuzurura hapa hapa nyumbani. Kama simba wangesonga mbele kidogo kwenye champion league basi Tanzania ingeongeza point kadhaa ambazo zingeiwezesha Yanga pia kushiriki champion league lakini sisi ni watanzania ujinga tumueweka mbele kuliko ujengaji.Yanga hao hao huangaika hadi kuifanya hujuma simba kwenye mechi zake za kimataifa ili isifike mbali yaani ni ujinga kabisa na roho mbaya zenye chembe ya hasada na uchawi tunafanyiana sisi wenyewe kwa wenyewe ili kuinufaisha timu ngeni wakati ambao tulitakiwa kusahau tofauti na kuunganisha nguvu zetu kwa manufaa ya taifa. Mechi za kimataifa ni kwa ajili ya kulijengea taifa heshima zaidi kuliko klabu ni vyema kwa wadau wa soka wakazingatia hilo na kuacha ushabiki wa kupumbavu .

    ReplyDelete
  4. hakika umenena kitu ambacho hata wewe ni miongoni mw wahanga na kisa si kingine ni kuchumia tumbo tu na masilahi binafsi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic