October 8, 2020


MCHEZO kati ya KMC na Yanga utakaopigwa Oktoba 25 utachezwa Uwanja wa CCM Kirumba baada ya wenyeji KMC kuomba iwe hivyo.

KMC yenye maskani yake Kinondoni imeomba mchezo huo uchezwe Mwanza badala ya Dar ambapo wamekuwa wakitumia Uwanja wa Uhuru na Mkapa kwa mechi zenye idadi kubwa ya mashabiki ikiwa ni pamoja na zile za Simba na Yanga.


KMC imecheza mechi tatu Uwanja wa Uhuru na imeshinda mbili dhidi ya Mbeya City kwa mabao 4-0 na ile dhidi ya Tanzania Prisons kwa kushinda mabao 2-1 huku ikipoteza mchezo mmoja kwa kufungwa bao 1-0 na Polisi Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 8 na Bodi ya Ligi Tanzania imeeleza kuwa kanuni inaziruhusu timu kuchagua mechi mbili ambazo watacheza kwenye uwanja wa chaguo lao (tofauti na uwanja wa nyumbani).

4 COMMENTS:

  1. Simba jipangeni uswahiba unawazidia yote hii ni kuogopa Yanga hata wahamishie kasarani Ni kupigwa tu

    ReplyDelete
  2. Hilo Timu mnageuza mnavyotaka hata wakucheza na Simba queen,Yakisikia Yanga mabega juu
    Tuta washusha Kama Lipuli

    ReplyDelete
  3. sasa timu ya kinondoni mechi wanaipeleka mwanza kwanini?

    ReplyDelete
  4. wamefanya maamuz sahii kwa ajili ya mapato

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic