KLABU ya Gwambina FC leo imepata ushindi wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi nne bila kuambulia ushindi kwenye ligi.
Ushindi wa leo imepata mbele ya Ihefu FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba baada ya Uwanja wa Gwambina Complex kufungiwa na Bodi ya Ligi Tanzania kwa kuwa haujakidhi vigezo.
Mabao yote ya Gwambina FC leo yamepachikwa kimiani na nyota wao Meshack Abraham dakika ya 33 na 48 na kuwafanya Ihefu wapoteze pointi tatu nyingine mzunguko wa tano.
Mchezo uliopita Ihefu FC iliacha pointi tatu mbele ya Mwadui FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mwadui Complex.
Gwambina kwenye mechi zake nne zilizopita ilikuwa haijawahi kufunga ndani ya dakika 360 hivyo leo imeambulia pointi zake tatu kwa mara ya kwanza kwa ushindi wa mabao 2-0.
Gwambina inafikisha jumla ya pointi nne kibindoni huku Ihefu ikibakiwa na pointi tatu kwa kuwa ilishinda mchezo mmoja mbele ya Ruvu Shooting.
Hakuna timu hapo wenye timu wenyewe mahasidi wakubwa na itafungwa hadi ligi ishe.
ReplyDelete