HIMID Mao mzawa anayekipiga ndani ya Klabu ya ENPPI ya Misri amesema kuwa kwa namna soka la Tanzania linavyokuwa kwa kasi ni rahisi kwa wachezaji wengi wazawa kupata timu nje ya nchi.
Himid ambaye pia aliitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Burundi amesema kuwa anafurahi kuona ushindani ndani ya Bongo unavyozidi kuwa mkubwa.
Aliibuka nchini Misri akitokea Klabu ya Azam FC ambayo leo imeibukia Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, utakaochezwa Oktoba 26, Uwanja wa Jamhuri, Moro.
Himid amesema:"Kwa namna ambavyo mambo yanakwenda ndani ya Bongo ninaona kwamba ushindani unazidi kuwa mkubwa na wachezaji wanajituma.
"Muhimu kuona kila mtu anatimiza ndoto zake na kupata fursa ya kufanya kile ambacho anakipenda inawezekana."
0 COMMENTS:
Post a Comment