KOCHA wa Klabu ya KMC, Habibu Kondo, amewatahadharisha Yanga kutokwenda na matokeo kichwani katika mechi dhidi yao itakayochezwa Jumapili ya tarehe 25 /10/2020 jijini Mwanza.
Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Oktoba 22, Uwanja wa Uhuru.
Kwa sasa kimeshatia kambi Mwanza kwa ajili ya mchezi wa ligi dhidi ya KMC utakaochezwa kesho saa 10:00 jioni.
Kondo amesema:-”Tunashukuru Mungu tumefika salama na kwa sasa tumeshakuwa wenyeji hapa Mwanza, tumepata nafasi ya kufanya mazoezi na tumefanya mazoezi kuanzia saa 9:00 hadi saa 11:00 jioni ili kuendelea kuzoea hali ya hewa, kiufundi timu tumeiandaa vyema.
Ameongeza kuwa; ”Yanga isijiamini na matokeo iliyoyapata katika mchezo wa mwisho dhidi ya Polisi Tazania, huku sisi tukitoa sare katika mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Ruvu Shooting, sisi tulikutana na wapinzani bora sana ndiyo maana tukapata matokeo hayo lakini dhidi ya Yanga ni mechi tofauti kabisa”.
KMC inajivunia kikosi chake chenye nyota kadhaa kama nahodha Juma Kaseja aliyepo kwenye kiwango bora kwa sasa, Israel Mwenda, Hassan Kapalata, Reliant Lusajo, Keny Ally Hassan Kabunda, Andew Vicent “Dante” na wengineo.
Katika msimu huu wa ligi 2020-2021, KMC ipo kwenye nafasi ya 6 ikiwa imecheza michezo 7, imeshinda 3 na kutoka sare 2, huku wakipoteza michezo 2 wakiwa wamefunga magoli 9 na kuruhusu kufungwa magoli 4.
”Tunashukuru Mwenyezi Mungu tumefika salama tangu jana, kwa sasa tumeshakuwa wenyeji hapa Mwanza, tumepata nafasi ya kufanya mazoezi jana na tumefanya mazoezi tena leo kuanzia saa 9:00 alasiri ili kuendelea kuzoea hali ya hewa, kiufundi timu tumeiandaa vyema”, alisema.
Ameongeza kuwa ”Yanga isijiamini na matokeo iliyoyapata katika mchezo wa mwisho dhidi ya Polisi Tazania, huku sisi tukitoa sare katika mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Ruvu Shooting, sisi tulikutana na wapinzani bora sana ndiyo maana tukapata matokeo hayo lakini dhidi ya Yanga ni mechi tofauti kabisa”.
KMC inajivunia kikosi chake chenye nyota kadhaa kama nahodha Juma Kaseja aliyepo kwenye kiwango bora kwa sasa, Israel Mwenda, Hassan Kapalata, Reliant Lusajo, Keny Ally Hassan Kabunda, Andew Vicent “Dante” na wengineo.
Katika msimu huu wa ligi 2020-2021, KMC ipo kwenye nafasi ya 6 ikiwa imecheza michezo 7, imeshinda 3 na kutoka sare 2, huku wakipoteza michezo 2 wakiwa wamefunga magoli 9 na kuruhusu kufungwa magoli 4.
Tatu kavu zinawasubiri
ReplyDelete