ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu amesema kuwa vijana wake wanaimarika taratibu hivyo anaamini kwamba mechi zijazo atapata matokeo chanya.
Kwa sasa Ihefu FC ipo nafasi ya 18 baada ya kucheza mechi nane na imekusanya jumla ya pointi nne kibindoni.
Imeshinda mechi moja ilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Sokoine kwa ushindi wa bao 1-0 na imefungwa jumla ya mechi sita ikiwa na sare moja mkononi.
Katwila ambaye aliibukia Ihefu akitokea Klabu ya Mtibwa Sugar amesema kuwa kuna makosa ambayo yanafanywa na wachezaji wake anaona taratibu yanapungua muda unavyokwenda.
"Ilikuwa ni ngumu kuanza kwa ushindi kwa kuwa wachezaji walikuwa hawajajiamini sana lakini kwa sasa naona mwendo wao sio mbaya, taratibu wanazidi kuimarika.
"Tuna mechi ambazo zipo mbele yetu, nimewaambia kwamba ni muhimu kujiamini na kucheza kwa mipango ya kupata ushindi, kila kitu kinawezekana kikubwa kujiamini na juhudi," amesema.
Mchezo wake wa kwanza kukaa benchi, Katwila alishuhudia timu yake ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Sokoine.
0 COMMENTS:
Post a Comment