October 25, 2020

 


VITA kubwa ni kwenye kusaka pointi tatu ndani ya uwanja na zile tatu bora ni balaa kwa sasa ambapo Azam FC ni baba lao wakiwa nafasi ya kwanza na pointi 21.

 

Mbali na vita ya pointi tatu, ishu ya mkwanja wanaovuta makocha waliopo ndani ya Bongo ni balaa, Yanga wanatamba na wadhamini wao Kampuni ya GSM huku Simba wakiwa na bilionea kijana, Mohamed Dewji, Azam FC ni matajiri wa Dar, wao wapo vizuri, hawana shida.

 

Championi Jumamosi limeingia chimbo kukuletea mkwanja wa makocha wa Bongo huku Sven Vandenbroeck na Aristica Cioaba wakiwafunika wote namna hii:-


SVEN VANDENBROECK


Kichwa chake kwa sasa kinampasuka kwa namna kikosi chake kipana kinavyopata tabu baada ya kuchezeshwa gwaride na Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela kwa kufungwa bao 1-0. 


Anatajwa kuvuta dola 9,000 ambazo ni sawa na Sh 20.7Mil kwa mwezi.

 

CEDRIC KAZE


 Ameanza kwa kuipa ushindi Yanga mbele ya Polisi Tanzania kwa timu yake kushinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania.


Ni Cedric Kaze raia wa Burundi anatajwa kulipwa dola elfu 7,800 ambazo ni sawa na Sh 18Mil.





ARISTICA CIOABA


Kocha huyu raia wa Romania ameanza kwa kasi yake ndani ya kikosi cha Azam FC na mpaka sasa timu yake ndiyo kinara kwenye ligi ikiwa imeshinda mechi zote saba anatajwa kuvuta dola 9,000 ambazo ni sawa na Sh 20.7Mil kwa mwezi.


 

MBWANA MAKATA


 Huyu ni Mtanzania na ni kocha wa Dodoma Jiji, mpaka sasa ikiwa ni raundi saba akiwa nafasi tano na pointi zake ni 12.


 Anatajwa kulipwa Sh 2Mil kila mwezi.

 

KHALID ADAM 


Kocha huyu mzawa mwenye mikwara mingi akiwa kazini pale Mwadui, kwa mwezi akaunti yake inatajwa kuvimbishwa kiasi cha Sh 1.8Mil.


MECKY MAXIME 


kocha wa Kagera Sugar, yeye anaingiziwa benki Sh 3Mil kila mwezi na jina lake wakati fulani lilitajwa kwenye rada za kutakiwa na Yanga akawe msaidizi.

 

FULGENCE NOLVATUS


 Akiwa ameipandisha timu ya Gwambina kutoka Ligi Daraja la Kwanza na sasa anapambana ndani ya Ligi Kuu Bara, inaelezwa kuwa mkwanja anaovuta mwisho wa mwezi Sh 2Mil.

 

AMRI SAID


Licha ya kwamba mwendo wake ulikuwa ni kusuasua ndani ya Mbeya City yenye maskani yake Mbeya huku ikitumia Uwanja wa Sokoine kabla ya kufutwa kazi Oktoba 20, inaelezwa kuwa alikuwa anavuta Sh 4Mil kwa mwezi.

 

ABDALAH MOHAMED ‘BARES’


Huyu ni kocha wa JKT Tanzania ambaye mambo kwake yanaenda mrama kutokana na timu kuwa na matokeo yasiyofurahisha mwisho wa mwezi anatajwa kuvuta Sh 3.5 Mil.


CHARLES MKWASA


Miongoni mwa wazawa ambao wanaufahamu vema mpira wa Bongo na uzoefu unambeba pia. Aliibukia Ruvu Shooting baada ya kumalizana na Yanga si haba inatajwa kuwa mwisho wa mwezi anavuta Sh 3Mil.

 

HABIB KIONDO


 Wana Kino Boys, KMC walianza kwa kasi isiyo ya kawaida na waliweza kuongoza ligi kwenye raundi tatu za mwanzo kwa sasa wanatafuta kurudi kwenye ramani. Licha ya mapito hayo, Kiondo anatajwa kuvuta Sh 3.5Mil.

 

HITIMANA THIERY


Ana kazi kubwa kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa kwa kuwa timu ya Namungo inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho. Mwisho wa mwezi anatajwa kuvuta Sh 3.5Mil.

 

SALUM MAYANGA


 Mwili jumba, Simba wanajua alichowafanya Uwanja wa Nelson Mandela baada ya timu yake ya Prisons kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Aliweza pia kuifundisha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Anatajwa kuvuta Sh 2.5Mil kwa mwezi.

 

ZUBER KATWILA

Alikuwa ndani ya Mtibwa Sugar, sasa yupo ndani ya Ihefu FC na inatajwa kuwa anavuta Sh 2Mil na mchezo wake wa kwanza kukaa benchi alipokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Azam FC.

 

MALALE HAMSINI

Yupo kwa sasa ndani ya Polisi Tanzania baada ya kufutwa kazi kwenye timu yake ya zamani ya Ndanda FC. Bado ana maumivu ya kunyooshwa bao 1-0 dhidi ya Yanga ya Cedric Kaze Uwanja wa Uhuru. Anatajwa kuvuta Sh 2Mil mwisho wa mwezi.


VINCENT BARNABAS

Kocha Msaidizi wa Mtibwa Sugar ambaye ameachiwa mikoba na Zuber Katwila ambaye ametimkia Ihefu, anatajwa kuvuta Sh 2Mil kwa mwezi.

 

JUMA MGUNDA

Akiwa ni mchezaji wa zamani wa Coastal Union na kwa sasa ni kocha mkuu ndani ya timu hiyo yenye maskani yake Mkwakwani, Tanga, anatajwa kulipwa Sh 1.5Mil kwa mwezi.

 

FRANCIS BARAZA

Akiwa zake ndani ya Biashara United anaendelea kufanya mambo yake huku akitajwa kulipwa Sh 2.5Mil mwisho wa mwezi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic