October 5, 2020


 MABOSI wa Klabu ya Simba wamewaondoa hofu mashabiki wake kwa kutamka kuwa kiungo wao Mzambia, Clatous Chama na mshambuliaji Mnyarwanda Meddie Kagere tayari wameanza kuandaliwa mikataba mipya ya kuendelea kubakia klabuni hapo.

 

Mastaa hao wote wamebakisha mwaka mmoja kila mmoja hadi kufikia usajili wa dirisha dogo wanakuwa wamebakisha miezi sita ambayo inatoa ruhusa ya kufanya mazungumzo na klabu nyingine itakayomuhitaji kwa mujibu wa kanuni za Fifa.


Tetesi za usajili zinasema kuwa, wachezaji hao huenda wakaihama timu hiyo mara baada ya mikataba yao kumalizika,kutokana na uwezo wao kuwa mkubwa kila iitwapo leo.



Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hakuna mchezaji yeyote atakayeondoka katika timu hiyo.

 

“Mengi yanazungumzwa kuhusiana na wachezaji wetu Chama na Kagere, ukweli ni kwamba hivi sasa uongozi upo kwenye mazungumzo ya mwisho na mameneja wa wachezaji wetu hao kwa ajili ya kuwaongezea mikataba.


"Kikubwa zaidi hao wachezaji wenyewe wameonyesha nia kubwa ya kuendelea kubakia kuendelea kuichezea Simba katika misimu mingine inayofuatia.

 

“Tunataka kuendelea kuwa na kikosi imara kitakachopata makombe, hivyo niwatoe hofu mashabiki Simba, hakuna mchezaji atakayeondoka bila klabu kutaka, wachezaji wote ambao tupo kwenye mazungumzo nao tumefikia hatua nzuri,” amesema Manara.


Chanzo:Championi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic