October 5, 2020


UONGOZI wa Azam FC, umesema kuwa mwendelezo mzuri wa matokeo ambayo wanayapata ndani ya Ligi Kuu Bara unatokana na maandalizi wanayoyafanya pamoja na uwezo wa wachezaji walionao.


Jana,Oktoba 4 kikosi cha Azam FC kiliendeleza rekodi yake ya kushinda mechi zake za ligi ikiwa ni mara yake ya tano baada ya kushinda kwa mabao 4-2 mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa hesabu kubwa kwa timu ya Azam ni kuendekea kupata matoke chanya kwenye mechi zetu zote.

"Mwendelezo mzuri ndani ya ligi ni jambo ambalo tunalihitaji kwa kuwa kikubwa ni kupata pointi tatu muhimu hilo ndilo jambo la msingi.

"Wachezaji wanatambua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo na wenyewe pia wachezaji wanahitaji kupata matokeo hivyo wanatimiza majukumu yao ndani ya uwanja," amesema.

Ushindi huo unaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 15 kibindoni na imefunga jumla ya mabao tisa huku ikifungwa mabao mawili kwenye ligi.


Mabao ya Azam FC yalifungwa na Prince Dube aliyetupia mawili dakika ya 6 na 88, Obrey Chirwa alitupia moja dakika ya 48 pamoja na Richard Djod dakika ya 51.

Kagera Sugar wao mabao yao yalifungwa na David Luhende dakika ya 33 na Yusuph Mhilu dakika ya 50.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic