October 11, 2020

 


MECKY Maxime amesema kuwa kwa sasa wachezaji wake wanaendelea kujinoa licha ya kwamba kuna mapumziko mafupi kutokana na timu za Taifa kuwa na mechi kimataifa zilizopo kwenye kalenda ya FIFA. 


Leo Oktoba 11, Timu ya Taifa ya Tanzania ina kazi ya kucheza na timu ya Burundi kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.


Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa kwa sasa bado wachezaji wake wapo kambini ikiwa ni kwa ajili ya kuendelea kujiweka fiti.


"Tunatambua kwamba kwa sasa kuna mapumziko mafupi ambayo yametokana na timu ya Taifa kuwa na mchezo na haki hii sio Bongo pekee hata Ulaya pia ipo.


"Lakini kuwa namna hiyo hakutufanyi tusiendelee kufanya maandalizi kwani mechi itachezwa siku moja hivyo ni muhimu kuipa sapoti timu yetu ya Taifa ya Tanzania lakini wachezaji wapo kambini na mapambano yanaendelea.


"Mchezo wetu ujao ni dhidi ya Namungo ni muhimu kujiweka fiti ukizingatia kwamba ushindani ni mkubwa msimu huu wa 2020/21," amesema. 


Kagera Sugar imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 4-2 dhidi ya Azam FC inakutana na Namungo FC iliyotoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Mwadui FC. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic