October 11, 2020

 


THOBIAS Kifaru Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar ambaye amefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 na akiwa ni miongoni mwa wafanyakazi makini ndani ya Bongo katika kutimiza majukumu yake amesema kuwa timu hiyo inarejea kwenye ubora wake mdogomdogo.


Kifaru ameweka bayana kuwa wamejipanga kuona msimu huu wakimaliza ndani ya nafasi tano za juu kukwepa  presha ya msimu uliopita ambapo iliponea chupuchupu kucheza playoff ama kushuka jumlajumla Ligi Daraja la Kwanza. 


Akizungumza na Saleh Jembe,  Kifaru amesema kuwa makosa ambayo waliyafanya msimu wa 2019/20 wameyafanyia kazi baada ya kusajili wachezaji wazuri ambao wanaamini watawapa matokeo mazuri.


"Kwa msimu wa 2019/20 kwetu sisi nasema ulikuwa ni msimu mbayambayambaya haijawahi kutokea nasema tena mbaya kwelikweli haijawahi kutokea kwani ilikuwa ni chupuchupu tushuke Daraja ama kucheza playoffs.


"Hatujaanza vizuri lakini tutafanya vizuri msimu huu kwani tumefanya usajili mzuri kwelikweli tuna washambuliaji wao wanaweza kufunga tu muda wote na kweli tutawafunga wengi msimu huu acha kabisa," amesema Kifaru


Mechi mbili Mtibwa Sugar imepoteza mfululizo,  ilianza kufungwa na Yanga kisha ikafungwa na Biashara United,  mechi zote ilifungwa bao mojamoja.


Kuendelea kujiandaa jana ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Geita Gold inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic