USHINDI wa Azam FC jana Oktoba wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC umewapa presha mabingwa watetezi Simba kwa kusema kuwa wanakikosi kizui kinachostahili pongezi.
Kwa sasa Azam FC ni vinara wa igi Kuu Bara wakiwa na pointi 18 baada ya kucheza mechi 6 ndani ya Ligi Kuu Bara imefunga jumla ya mabao 12 huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano na imefunga mabao 14.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika namna hii:- "Kwa mwenendo huu ,naiona Azam FC ikipigania taji msimu huu.
"Mna kikosi kizuri na kwa kweli mnastahili hongera.Timu inayopigania mataji huwa hailalamiki lalamiki hovyo, huwaoni na makabrasha TFF wala FIFA au CAS.
"Hamkupokea mchezaji kwa mbwembwe bandarini wala stendi ya Ubungo, lakini mnaonyesha how serious you are.(Namna gani mpo makini)."Najua msimu huu mtakamata nafasi ya pili nyuma ya champion wa taifa hili, yule wa tatu mtamuacha kwa Pointi ishirini na tano,"
Pressure gani?raund ya kwanza haijaisha?wacha team kubwa zikutane kwanza tutajua mwelekeo.
ReplyDeleteNaam hawalalamiki, Hawana Kesi, hawapugi, hawachani nguo za wapinzani, hwabughudhi wachezaji wao na wala hawana zomeazomea. Wanacheza mpira wa mzuri tena wa kuvuta na wanastahiki kila kizuri
ReplyDeleteKuna timu hapa bongo inajihisi yenyewe ndo inastahili kuchukua kombe la ligi kuu ndo mana malalamiko hayaishi badala ya kucheza mpira uwanjanai wao kila siku ni malalamiko tu, wanafikiri hiki ni kipindi cha malinzi
ReplyDeleteMuendeleze mchezo wa kiizi...wamanga shida tupu!!
ReplyDelete