LEO Oktoba 16 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ambapo mchezo mmoja utachezwa kwa timu mbili kusakapointi tatu muhimu.
Dodoma Jiji FC itawakaribisha Mbeya City Uwanja wa Jamhuri Dodoma saa 10:00.
Dodoma Jiji ipo nafasi ya saba kwenye msimamo baada ya kucheza mechi tano na mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mwadui FC msimu wa 2020/21 ilishinda bao 1-0.
Imekuwa na matokeo chanya Uwanja wa nyumbani jambo linaloongeza ugumu kwa Mbeya City ambayo imekuwa kwenye mwendo wa kusuasua kwa msimu wa 2020/21.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi tano za ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment