LEO Oktoba 14 Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea ikiwa ni raundi ya sita baada ya raundi tano kumeguka huku Azam FC wakiwa ni vinara na pointi zao 15.
Leo mambo yatakwenda namna hii:-
Biashara United iliyo nafasi ya 6 na pointi 10 itawakaribisha Ihefu iliyo nafasi ya 17 na pointi 3, Uwanja wa Karume, Mara saa 10:00 jioni.
JKT Tanzania iliyo nafasi ya 16 na pointi 4 itawakaribisha Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 12 na pointi 5, Uwanja wa Jamhuri Dodoma saa 8:00 mchana.
KMC iliyo nafasi ya 7 itawakaribisha Coastal Union iliyo nafasi ya 15 na pointi 4 Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni.
Namungo FC iliyo nafasi ya 9 na pointi 6 itawakaribisha Kagera Sugar iliyo nafasi ya 13 na pointi 4 Uwanja wa Majaliwa saa 10:00 jioni.
0 COMMENTS:
Post a Comment