October 29, 2020

 


ALIYEWAHI kuwa kocha wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amemtaja kocha wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck kuwa ndio chanzo cha matokeo mabaya kwenye michezo miwili iliyopita.

 

Simba imepoteza mchezo wa pili mfululizo baada ya awali kufungwa dhidi ya Tanzania Prisons bao 1-0 kisha Ruvu Shooting bao 1-0, ikiwa nafasi ya nne ya msimamo wa ligi ikibaki na pointi zake 13, baada ya kucheza michezo saba.


Sven ambaye alifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita, alianza vizuri ligi ya msimu huu wa 2020/21, kwa kushinda michezo minne na kutoa sare moja, lakini mambo yameanza kuharibika katika michezo miwili iliyopita huku majeruhi yakitajwa kuwa tatizo.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Julio alisema kuwa, Kocha Sven alifanya makosa awali kwa kuwataka waamuzi kuwalinda wachezaji wake mastaa jambo ambalo limewapa kichwa hivyo kusababisha matokeo haya kwa kujiona wao ni bora kuliko wengine.



“Mwalimu alifanya makosa kwa kusema wachezaji wake ni mastaa na waamuzi wawalinde, naamini wachezaji mastaa wanalindwa lakini kwa levo ya mastaa wa Simba bado hawajafikia huko.

 

“Sasa lile ni tatizo kwa wachezaji, unawapa sifa ambayo hawana wachezaji wanaotakiwa kulindwa kwa Afrika kama vile kina Didier Drogba, Samuel Eto’o na wengineo siyo hawa.

 

“Unavyosema hivyo unawaweka wachezaji wako kwenye levo kubwa ambayo hatujafikia, hivyo inapelekea wakajiona bora zaidi kuliko wachezaji wengine, hivyo ni vyema wachezaji wakajiangalia na kujitathmini, japo naamini Simba ni timu kubwa ina uwezo mzuri na inaweza kufanikiwa kutwaa ubingwa msimu huu,” alisema Julio ambaye ni kocha wa timu ya vijana chini ya miaka 20.

4 COMMENTS:

  1. Nadhani kosa kubwa la Sven ni kutowapa nafasi baadhi ya wachezaji akiwaami wengine. Sasa matokeo yake wale anaowaamini wamekua majeruhi. Ni ngumu mno kwa mchezaji ambae humuamini kuweza kukupa matokeo chanya kwa sababu ya kukosa uzoefu. Inabidi benchi la ufundi liwape nafasi ya kucheza wachezaji wote waliosajiliwa msimu huu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umeongea kiufundi kuliko mropokaji anayejiita kocha wakati kila timu akipewa inafanya vibaya

      Delete
    2. Hoja yako ni ya msingi.Wachezaji wa Simba Kwa asilimia 90 wanalingana viwango hivyo Kwa mantiki hii inabidi awape rotation wachezaji wote kucheza.Unamuweka mchezaji benchi mechi tano mfululizo na unamchezesha mechi ya sita tena baada ya hawo kuwa majeruhi..unategemea atapeform?...mechi za kirafiki hazina ushindani na uzoefu unaonyeasha wachezaji hawajitoi Kwa kuogopa kuumizwa na hii ilijionyesha mechi za Simba za kirafiki kama African Lyon,Transist Camp, KMC,Mlandege.
      Kocha aache kukariri kucheza wachezaji hawo hawo vinginevyo tutakuja kuwapoteza kina David Kameta, Ame Ibrahim,Miraj Athuman,Michael Gadiel Michael, Ibrahim Ajib nk kama tulivyo shuhudia viwango kushuka kina Rashid Juma,Yusuf Mpilipili.Ingekuwa bora awe anawapa nafasi hata dk 20 na sio dk 5 za kucheza hizo mechi za VPL.

      Delete
  2. Kufungwa simba nini cha ajabu na kuanza kumsengenya kocha? Huu ushindani ni mzuri na kwa simba nnaimani kocha wa simba ni miongoni mwa makocha wenye furaha kubwa kwa sasa kwani alihitaji na anahitaji kukitafakari kikosi chake Kabla ya Klabu bingwa Africa. Ausems alifeli na simba klabu bingwa Africa msimu uliopita kwa sababu alikosa muda wa kujua mapungufu ya timu yake. Lakini Kama marefa wangekuwa makini simba hii isingekuwa na majeruhi kiasi hiki. Wachezaji wa simba wanapigwa kweli kweli kisa wanacheza mpira mzuri. Kapigwa morisoni,kanyimwa penalt kadhaa sababu nini? Haijulikani. Sven Kama kocha wa simba haki yake kuwatetea wachezaji wake Julio hana uwezo wa kumkosoa kocha wa simba anatafuta sifa tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic