October 6, 2020


KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakichezewa faulo mbaya ndani ya uwanja jambo ambalo linampa hofu.


Kwa sasa timu za Simba ipo kwenye mapumziko ya muda kutokana na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kuweka kambi Oktoba 5 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 11 Uwanja wa Mkapa.

 Miongoni mwa nyota wa Simba ambaye kwa sasa anatibu majeraha aliyopata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United, Uwanja wa Mkapa.

Ipo nafasi ya pili kwenye ligi ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi 5 za ligi na kinara ni Azam FC mwenye pointi 15. 

Sven amesema:“Wachezaji wangu wanachezewa rafu mbaya ambazo zinaweza kuwaumiza vibaya na kuiathiri timu. Lazima wahusika wawe macho.Ligi bado mbichi hii.

"Kuanza kupata majeruhi mapema inaweza kutuathiri sana. Waamuzi wawe macho na pia wachezaji wa timu zote watambue soka ni burudani sio vita."


1 COMMENTS:

  1. Vizuri sana coach lazima wajue mpira ni mchezo wa burudani sio ugomvi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic