KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije ameeleza sababu za kuacha kuwaita mabeki wa pembeni wa Klabu ya Yanga Kibwana Shomari na Yassin Mustapha ni mfumo wa timu na matumizi waliyopewa ndani ya Yanga.
Ameeleza mfano wa mabeki wa KMC Israel Mwenda na Brayson David ni wachezaji ambao wametengeneza nafasi nyingi za kufunga na pia wametengeneza mabao (Assist) za kutosha hivyo ndio sababu kubwa iliyofanywa kuitwa.
Taifa Stars inajiandaa na mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Burundi unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 11 na kwa sasa tayari timu imeshaingia kambini kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mwisho.
Wachezaji ambao wameitwa kutoka Yanga ni pamoja na Feisal Salum, Ditram Nchimbi na Bakari Mwamnyeto.
0 COMMENTS:
Post a Comment