October 17, 2020


ALIYEKUWA Kocha wa Yanga, Mserbia, Zlatko Krmpotic ameibuka kuwa ameamua kwenda mwenyewe kwa miguu yake katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kuishitaki Yanga kutokana na kitendo cha uongozi wa klabu hiyo kuvunja mkataba wake bila kuwepo makubaliano yoyote.

 

Hivi karibuni, Yanga ilitangaza kumfuta kazi kocha huyo kutokana na kile kilichoelezwa timu kucheza kwa kiwango cha chini licha ya kushinda mechi zake, ambapo kwa sasa kazi ya kukinoa kikosi ipo kwa Mrundi, Cedric Kaze aliyetua Oktoba 15 Bongo akitokea Canada.


Akizungumza na Championi IJumaa, Krmpotic alisema kuwa uongozi wa timu hiyo umevunja mkataba wake lakini hakuna makubaliano yoyote ambayo walisani, jambo ambalo halipo kitaaluma, hivyo ameamua kwenda FIFA mwenyewe baada ya kuwafungulia kesi ya madai ya fedha zake.

 

“Hadi leo (juzi) hawajasaini makubaliano yoyote ya kuvunja mkataba, hawajali kwa sababu wanajua fedha ninayowadai haitalipa klabu.

 

“Lakini atalipa bosi wao ambaye anafadhili kila kitu. Niliwashtaki FIFA na katika siku chache zijazo nitaenda mwenye makao makuu ya FIFA huko Zurich kwa ajili ya hili jambo hawajanitendea haki,” alisema Krmpotic.

5 COMMENTS:

  1. Uto ni Wadaiwa sugu 😀😀

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dah chama langu Yanga! Hivi Luc Eymael naye mlishamalizana naye au atajiunga na huyu kudai?

      Delete
  2. Haya ndio matatizo ya kumwachia mfadhili kila kitu mwisho wa siku klabu ndio inachukuliwa hatua

    ReplyDelete
  3. Haya tumekusikia lkn ngoja vyura wamkee usikie watakavyokoroma kuwa kuna mkono wa Simba

    ReplyDelete
  4. Unajua ukiwa na jirani mwanga Amani hupati, kwani yeye wa kwanza,je Kocha wa Ihefu naye kaenda Fifa?Salehe Buana tumetulia Wananchi majungu ya nini?au Saidio anakuchangaanya , zingatia bado nafasi moja ya Maproo .Au wewe dalali wake ,Kuna kipindi uliandika Hassan Kessy anadai Yanga je alilipwa?.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic