October 17, 2020

 


BEKI wa Klabu ya Ihefu FC, Omary Kindamba atakuwa nje kwa muda wa  wiki tatu hadi nne kufuatia  nyota huyo kupata majeraha ya mbavu baada ya kuanguka vibaya alipokuwa akiitetea timu yake dhidi ya Biashara, Mara.


Mchezo huo uliochezwa Oktoba 14, Uwanja wa Karume Ihefu ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.


Ihefu ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu imekuwa na mwendo wa kusua ipo nafasi ya 17 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 6.


Imekusanya pointi tatu kwa kuwa ilishinda mchezo mmoja dhidi ya Ruvu Shooting kwa kufunga bao 1-0 baada ya hapo mechi zake tano imepoteza.


Imefungwa jumla ya mabao saba na kufunga mabao mawili ndani ya msimu huu wa 2020/21.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic