October 14, 2020

 


MAPINDUZI Balama, kiungo mzawa anayekipiga ndani ya Yanga baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa muda mrefu taratibu ameanza kurejea kwenye ubora wake.


Daktari wa timu ya Yanga ameweka wazi kuwa muda mfupi kuanzia sasa kiungo huyo ambaye msimu uliopita aliingia kwenye orodha ya wachezaji waliofunga mabao bora atarejea kazini.


Bao lake moja kati ya matatu aliyofunga ndani ya Yanga kwenye Ligi Kuu Bara kabla ya kupata jeraha  katika kifunda cha mguu msimu uliopita Juni, mwaka huu alimtungua mlinda mlango namba moja wa Simba Aishi Manula akiwa nje ya 18 Januari 4, kwenye sare ya kufungana mabao 2-2.


Shecky Ngazija, daktari wa Yanga amesema kuwa hali ya kiungo huyo inaendelea vizuri na tayari ameshaanza kuufanyia mazoezi mguu wake jambo linalotoa matumaini ya kurejea kwake ndani ya uwanja hivi karibuni.


"Balama Mapinduzi anaendelea vizuri tangu kaumia kiwiko cha mguu wa kushoto miezi mitatu iliyopita, wiki iliyopita tulimfanyia vipimo vya mwisho ambavyo vinaonyesha kwamba yupo tayari kuanza kufanya mazoezi mepesi.


"Jambo la kufurahisha ni kwamba Balama ameshaanza kufanya mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa madaktari na ikiwa mambo yatakwenda sawa basi tunatarajia kumuona akicheza mechi zijazo," amesema. 


Yanga na Simba zilipaswa kukutana Oktoba 18 ila mchezo huo uliota mbawa na sasa utapigwa Novemba 7, Uwanja wa Mkapa.

3 COMMENTS:

  1. Lakini sasa inavoonesha mmeshasita kumsifu Morrison kwa kumtaja kila kuitaja bao lake alilolifunga kwa kumtenguwa Manila. Huenda mnangoja arudishwe tena Yana na muanze kulikunbuka tena

    ReplyDelete
    Replies
    1. inahusu nini habari ya goli la morisson na kupona kwa Balama

      Delete
  2. Ndio tatizo la mwandishi kwa sababu ni mwanachama wa vyura anajisahau hadi kwenye kazi yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic