October 3, 2020


 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kwa sasa hana presha kubwa kuelekea kwenye mechi yake ya ligi dhidi ya Yanga na badala yake anazitazama mechi zake za karibu.

Simba ina kazi ya kumenyana na Yanga ambao ni watani zao wa jadi, Oktoba 18, Uwanja wa Mkapa zikiwa zimebaki siku 14 kabla ya kukutana uwanjani.

 Sven amesema kuwa wachezaji na timu kiujumla ina kazi kubwa ya kusaka pointi tatu kwenye mechi zote watakazocheza jambo linalomfanya afikirie mechi zake za karibu kwanza.

“Tupo na mechi ngumu na nyingi ndani ya ligi, kabla ya kukutana na wapinzani wetu wengine tuna mechi  zipo karibu hivyo tunaanza kufikirikia kwanza mechi za mwanzo tukishamaliza kucheza hizi ndipo tutaanza kufikiria kuhusu Yanga.

“Malengo yetu ni kuona kwamba tunashinda taji la ligi kwani hilo lipo wazi na tumeanza na mipango hiyo mwanzo kabisa hivyo tunapambana kufikia malengo,” amesema Sven.

Simba kesho ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya JKT Tanzania mchezo utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma majira ya saa 10:00 jioni.


Inakutana na JKT Tanzania ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Coastal Union huku Simba ikiwa imetoka kushinda kwa bao 3-0 mbele ya Gwambina FC.  





1 COMMENTS:

  1. Mwenyezimungu tujaalie kesho tushinde ushindo mkubwa wa goli nyingi baada ya hapo tukutane na hao GONGOWAZI nao wale 5 zinawatosha inshaallah

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic