MBWANA Samatta amewasili leo kwa ajili ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania inayojiandaa na mchezo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Burundi, Oktoba 11.
Samatta kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya Fenerbahce ambayo inashiriki Ligi Kuu ya nchini Uturuki na tayari amecheza mechi mbili akiwa ametupia mabao mawili.
Samatta amesema kuwa anaamini Tanzania itapata matokeo chanya kwenye mchezo huo wa kirafiki.
"Utakuwa mchezo mgumu na nina amini kwamba mwalimu atakuwa na mpango mkubwa katika kutupa matokeo."
Taifa Stars inayonolewa na Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije iliangia kambini Oktoba 5 ikiwa ni tayari kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment