IMEELEZWA kuwa Cedric Kaze ndiye Kocha Mkuu wa Yanga ambaye atarithi mikoba ya Zlatico Krmpotic ambaye alifutwa kazi rasmi Oktoba 3.
Kwa sasa timu ya Yanga ambayo inajiandaa na mchezo wa dabi dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 18 ipo chini ya kocha msaidizi Juma Mwambusi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ndani ya Yanga ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga amesema:"Tulimuondoa Zlatico kwakuwa tulikuwa haturidhishwi na mpira wake, falsafa yake na mengine. Kwa sasa timu itakuwa chini ya Mwalimu Juma Mwambusi mpaka hapo kocha mpya atakapokuja.
"Miongoni mwa wale ambao tumewapa kipaumbele ni pamoja na Kaze kwa kuwa alikuwa ni chaguo letu la kwanza mwanzo. Ila kwa sasa bado kuna mambo tunakamilisha yakiwa sawa mashabiki watajua."
Zlatico aliongoza Yanga kwenye mechi 8 ambapo katika hizo zilikuwa tano za ligi na tatu za kirafiki. Kwenye mechi za kirafiki alishinda zote tatu na kwenye mechi za ligi alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons huku nne akishinda.
0 COMMENTS:
Post a Comment