October 4, 2020


 JANA, Oktoba 3, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic alifungashiwa virago vyake ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kukiongoza kikosi hicho kwenye mechi 8 za ushindani.

Kocha huyo alikiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi tano za Ligi Kuu Bara na aliongoza kikosi hicho kwenye mechi tatu za kirafiki na kwenye mechi za kirafiki zote alishinda kwa mabao mawili mawili.


Aliwasili nchini Agosti 29 na kuanza kazi kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi na alishinda kwa mabao 2-0.


Kwa sasa kikosi cha Yanga kilichotoka kushinda kwa mabao 3-0 mbele ya Coastal Union kipo chini ya Kocha Msaidizi Juma Mwambusi ambaye amepewa jukumu ya kukinoa kikosi hicho kinachojiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.


Habari zinaeleza kuwa miongoni mwa majina yaliyopo mikononi mwa Yanga ni pamoja na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Kaizer Chiefs, Ernst Middendorp ili abebe mikoba ya Krmpotic.


Ernst ni raia wa Ujerumani kwa sasa yupo Afrika Kusini akimalizia masuala ya kukabidhi ofisi kwa waajiri wake waliomfuta kazi.

12 COMMENTS:

  1. Ernst Middendorp sio kocha wa kuibadili Yanga. Amefukuzwa Kaizer Chiefs kwa matokeo mabaya. Tutabadilika lini?

    ReplyDelete
  2. Kafutwa kazi huko ndio anakujakuwa kocha wetu hapa. Tmetupa bunduki na badili yake Panga la bei chee. Tutaona mengi

    ReplyDelete
  3. Emmly alifukuzwa alikotoka mkamwokota na hakudumu mkafukuza nanyi pia, tafuteni makocha wanaoeleweka. Watumwe skaut wanaojielewa wampata tu kocha anayejua. Mtazamo wangu tu senzo asiwadanganye mkaingia chaka kuhusu makocha mtalia. Tuliieni tafuteni makocha kwa vigezo vyenu vya miaka yenu yote lkn kumbukeni ghorofa haliinuliwi kwa siku moja.

    ReplyDelete
  4. Ili uajiri kocha lazima awe amefutwa kazi sehemu fulani.
    Duniani kote mfumo ni huo.
    Wachache sana wanachukua walimu wachanga wanaotoka mafunzoni au wametoka mafunzoni wakafanya kazi club fulani harafu wakaajiriwa kwingine
    Kufukuzwa haina maana ni m bovu hawezi kazi.
    Ona akina Mourinho.
    Hata Liverpool wakimwajiri Klop akiwa ametimuliwa na Borrusia Dortmund.
    Hivyo Kama ataajiriwa huyo Mjerumani mwacheni aje.

    ReplyDelete
  5. Wajinga hao wameshinda mechi 3 droo 1 wanafukuza kocha wekeni mungine haraka ili nae mufukuze tarehe 18 tena akili za vyura aka kandambili aka GONGOWAZI

    ReplyDelete
  6. Hakuna kocha anayeelewa kwenye nchi ambayo mashabiki wanapanga kikosi chao.
    Kwani Simba walimfukuza Uchebe kwa shida gani kubwa?
    Tutamwamini au tutawaamini tuliowapa majukumu.
    Wakishindwa tutawavua madaraka.(wale tunaowamudu)

    ReplyDelete
  7. Senzo kaanza kazi rasmi kuijenga utopolo.

    ReplyDelete
  8. Hao makocha waliosoma kozi za ukocha miaka ya tisini hawawezi kwenda na kasi ya mabadiliko ya soka la kisasa. Na kwa nini viongozi wamemfukuza kocha wakati bado hawajapata kocha mwingine? Au wanatafuta kisingizio cha tarehe 18?

    ReplyDelete
  9. Sasa ww fyatu chukulia tarh 18 ukapigwa c utavnja tena vti kwa mpkapa acha kuingia na matokeo mezan ule ni mpira jana liverpool kapgwa 7 na vila ww ukija kupgwa 8 c utakufa

    ReplyDelete
  10. Acha aje huenda nyota ikang'aa yanga, ligi zinatofautiana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic