October 4, 2020


 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, leo Oktoba 4 kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mabao ya Simba yalifungwa na  Meddie Kagere aliyefunga mabao mawili dakika ya 4  na dakika ya 40 na mabao mengine yalifungwa na Chris Mugalu dakika ya 6 na Luis Miquissone  naye alitupia bao dakika ya 51. 

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 13 ikiwa nafasi ya kwanza na ina mabao 14 kibindoni huku nafasi ya pili ikiwa mikononi mwa Yanga yenye pointi 13 tofauti kwenye idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa. 

Yanga imefunga jumla ya mabao 7 kibindoni na ushindi wa jana, Oktoba 3 ulikuwa ni wa kwanza kwa Yanga kushinda mabao zaidi ya mabao 3 uwanjani.

2 COMMENTS:

  1. Yanga imeshinda kwa ushindi wa zaidi ya mabao 3???
    Uandishi hauwezi kuwa taalamu ngumu hivyo hata mtu kushindwa kuandika sentensi inayoeleweka.

    ReplyDelete
  2. Basi nyinyi yanga ndio mnaongoza hizo goli 14 zetu tunawapa nyinyi kandambili ili muongoze ligi akili zenu za matopeni kipi kibaya alicho andika mwandishi subirini tarehe 18

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic