October 17, 2020


 YANGA inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze baada ya kusaini dili la miaka miwili, jana Oktoba 16 mtambo wa kutengeneza mabao Kwenye kikosi hicho ni Carlos Carinhos raia wa Angola.


Kiungo huyo amehusika Kwenye mabao matatu kati ya saba ambayo  yamefungwa na Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara.


Alimpa pasi zote mbili Lamine Moro ilikuwa ni Kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City na Mtibwa Sugar wakati Yanga ikishinda bao 1-0  Kwenye mechi zote mbili.


Bao lake la Kwanza alifunga Oktoba 3 Uwanja wa Mkapa wakati Yanga ikishinda mabao 3-0 alipewa pasi na Deus Kaseke. 


Kwenye mechi hizo tano za Ligi Kuu Bara, Yanga ilikuwa inanolewa na Kocha Mkuu,  Zlatko Krmpotic ambaye alifutwa kazi Oktoba 3.

7 COMMENTS:

  1. Shingi ngapi huwa unalipwa ya kusifia uwozo huwo

    ReplyDelete
  2. Acha nicheke tuu. Asisti mbili na goli moja ndio mtambo wa magoli. Vipi Dube wa azam?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Azam unaijua wewe. Wamecheza juzi hakuna aliyekuwa na habari nao ila Yanga na Simba ndo kila kitu. Hata mechi za kirafiki za Yanga na Simba waulize hao Azam nani anamlipa mwenzie. Mbona mechi za kirafiki za timu nyingine hawazionyeshi live? Msiipe Azam ukubwa ambao hana. Tens Azam FC haina mdhamini Bali Bakhresa anatoa pesa mfuko wa kushoto anaweka mfuko wa kulia

      Delete
  3. Kichwa nazi... anazungumzia ndani ya Yanga. Kiwewe chako kinakupeleka kwa Dube.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utopolo peleka hko, Kama ww inataka wazungumzwe utopolo tu bila kuusuianisha wengine tembelea web ya utopolo hku unafuata nn. Emmy alisema utopolo viazi Ni viazi kweli

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic