CHRIS Mugalu, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa hesabu kubwa kwa washambuliaji wa kikosi hicho ni kuendeleza makali yao ya kufunga wawapo ndani ya uwanja huku akimuomba mlinda mlango wao Aishi Manula kutokufungwa kwenye mechi zake akiwa langoni.
Simba ikiwa imecheza mechi tano na kujikusanyia pointi 13 huku ikiwa nafasi ya pili imefunga jumla ya mabao 14 na kufungwa mabao mawili.
Kwenye idadi hiyo ya mabao Mugalu alifunga matatu kwenye mechi zake tatu ambazo amecheza mfululizo ikiwa ni mbele ya Biashara United, Gwambina FC na JKT Tanzania.
Ilifungwa mabao hayo kwenye mechi dhidi ya Ihefu kwenye ushindi wa mabao 2-1 na ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mugalu amesema:"Kabla ya mechi nimekuwa nikiongea na Manula na nimekuwa nikimsisitiza mara nyingi asiache lango likawa kwenye hatari ya kufungwa.
"Namhsukuru Mungu amekuwa akifanya hivyo kwani hata akifungwa ni idadi ya mabao ambayo hayazidi mawili.
"Mimi ninaona kwamba ana kazi ya kulinda lango huku sisi washambuliaji tukiwa na kazi ya kufanya ndani ya uwanja kumpunguzia presha na kufunga," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment