FC, Khalid Adam amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC utakaochezwa Oktoba 15, Uwanja wa Azam Complex.
Mwadui FC imetoka kushinda kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Namungo Uwanja wa Majaliwa inakutana na Azam FC ambayo imetoka kushinda mabao 4-2 dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo wao uliopita wa kujiweka fiti kwa ajili ya mechi zao za ligi ilicheza dhidi ya Yanga na ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 lililopachikwa kimiani na Michael Sarpong, dakika ya 81 ilikuwa ni Oktoba 9, Uwanja wa Azam Complex.
Adam amesema:"Wachezaji wapo vizuri na maandalizi yapo sawa matumaini yetu ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri ambayo yatatufanya tuzidi kuwa kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo.
"Ligi ina ushindani mkubwa kwa sasa hilo lipo wazi na kila mmoja anajua hivyo nasi ni lazima tufanye vizuri kupata matokeo.
"Tunakutana na timu bora hilo hakuna ambaye hajui ila nasi pia tupo vizuri, kuanza vibaya haina maana kwamba wachezaji hawana uwezo wa kupata matokeo," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment