October 13, 2020

 




KOCHA mkuu mpya wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze ambaye alitarajiwa kutua usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, sasa atatua Jangwani Oktoba 15 akitokea Canada kwa ajili ya kuanza kazi.

 

Awali iliripotiwa kuwa, Kaze angetua nchini Jumamosi pia ikaelezwa kuwa anaweza kutua Jumatano  alfajiri kwa ajili ya kuanza kazi Yanga lakini Jumamosi  habari kutoka ndani ya Yanga zilisema kocha huyo atatua Alhamisi na kuanza kazi katika kikosi hicho ambacho kipo kambini huko Avic Town, Kigamboni jijini Dar.

 

 Chanzo kilisema kuwa, kimefanya mawasiliano na kocha na kumwambia kuwa atatua nchini Alhamis  tayari kwa kuanza kazi.

 

“Kocha atakuja Alhamis akitokea Canada, akifika tu atamaliza masuala yake binafsi na uongozi, baada ya hapo ataanza kazi,” kilisema chanzo hicho.


Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga amesema:-" Kocha anatarajiwa kutua nchini Oktoba 15 Uwanja wa ndege wa kimataifa kila kitu kikiwa sawa."


 Kaze anatajwa kuja kuchukua mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye alifutwa kazi Oktoba 3 kwa kile kilichoelezwa kuwa falsafa yake haiendani na kasi ya Yanga.


Wakati anafutwa kazi alikiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi tano na ilishinda mechi nne na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons. 


Kinara wake wa mabao ni Lamine Moro ambaye ni nahodha mwenye mabao mawili huku timu ikiwa imefunga mabao saba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic