October 14, 2020


 WAKATI Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ikiwa imecheza jumla ya mechi tano ndani ya Ligi Kuu Bara kuna mitambo minne ya kazi imekuwa na uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza panga pangua.


Nyota hao ni Joash Onyango, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein na kipa namba moja Aishi Manula ambao wote wapo kwenye safu ya ulinzi. 


Licha ya Simba kutamba kwamba ina kikosi kipana ila kwa hawa jamaa imekuwa ni ngumu kuona wakikosekana kikosi cha kwanza msimu wa 2020/21.


Mechi ambazo walianza kikosi cha kwanza jumlajumla ilikuwa ni dhidi ya Ihefu Uwanja wa Sokoine, Mbeya ambapo Simba ilishinda mabao 2-1, kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Moro.


Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Biashara United ya Mara na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Gwambina ya Mwanza hizi zilipigwa Uwanja wa Mkapa.


Ngoma ilipokwenda Dodoma, Oktoba 4 kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Jamhuri, Dodoma mitambo ya kazi kama kawaida ilianza kikosi cha kwanza.


Vandenbroeck, amesema :"Wachezaji wote wanaocheza safu ya ulinzi ni watu wanaocheza kwa umakini na wanafanya kazi ngumu na kubwa na bidii yao inaonekana ndio maana inakuwa ngumu kubadili kama hawajapata majeraha.


"Haimaanishi wengine wanakosa nafasi ya kuanza siyo wachezaji wazuri hapana ni utaratibu tunaweka, lakini kazi ya Kapombe, Onyango ni nzuri bila kumsahau Manula na Tshabalala," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic