KIUNGO Ramadhan Chombo,' Redondo' anayecheza ndani ya Biashara United bado amekuwa kwenye ubra wake akiwa ndani ya uwanja kwa kucheza timu na kutengeneza mipango ya kufunga ili kuipa ushindi timu yake.
Biashara United ikiwa imefunga mabao matatu yeye amehusika mwenye bao moja ambapo alitoa pasi ya bao na kuipa pointi tatu muhimu timu yake.
Alitoa pasi yake nje ya wakati Biashara United ikishinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Kwa sasa Biashara United ipo nafasi ya 6 ina pointi 10 kibindoni.
Mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Ihefu FC utachezwa Oktoba 14.
Bao lilipachikwa na Kelvin Friday.
0 COMMENTS:
Post a Comment