INJINIA Hers Said Mjumbe wa Kamati ya Usajili ndani ya Klabu ya Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM amesema kuwa sababu ya kumfungia virago Kocha wao Zlatko Krmpotic ni kushindwa kuwa na uwezo wa kufikia malengo ambayo walikuwa nayo.
Oktoba 3 baada ya Yanga kushinda kwa mabao 3-0 mbele ya Coastal Union uongozi wa Yanga ulitangaza kufikia makubaliano ya kuachana na kocha wao jumlajumla.
Hersi amesema:- "Jambo la kumshukuru Mungu kwamba tumepata ushindi wa mabao mengi kwenye mechi yetu ya kwanza kwa msimu huu.
"Tuna kikosi kizuri msimu huu na muunganiko wa wachezaji wengi wazuri ambao wanaweza kutupa matokeo mazuri kwa kuwa kuna muunganiko mzuri.
"Kazi kubwa ilifanyika ili kumpata mwalimu na tulimpa malengo ambayo tulikuwa tunayahitaji na malengo hayakuwa kupata tu ushindi bali kuna mambo ambayo tulikuwa tunayafuatilia.
"Moja kati ya mambo ambayo tulikuwa tunayatarajia ni kupata matokeo mazuri ila hatukuridhishwa na falsafa ya mwalimu, aina ya uchezeshaji wake kwa wachezaji.
"Tulipoona hatujaridhishwa naye tulikaa naye chini na kuzungumza naye kwa namna ambavyo mwenendo wake ulikuwa hatukurishishwa kwa namna ambavyo alikuwa anakwenda, hivyo tukafikia makubaliano ya kuachana naye." amesema.
Zlatko ameacha timu ikiwa nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza baada ya kufikisha pointi 13 ila kwa sasa ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi zake hizohizo 13 na kinara ni Azam FC ambaye ana pointi 15. Oktoba 3 alishuhudia wachezaji wake watatu ambao ni Carlos Carlinhos, Haruna Niyonzima na Yacouba Songne wakipachika mabao yao kwa mara ya kwanza ndani ya ligi msimu wa 2020/21.
Na alikuwa akiandaa pacha kati ya Tusila Kisinda na Tonombe Mukoko ambayo iliwahi kumpa pointi tatu kwenye ushindi wa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba.
Yanga wapuuzi hakuna Sababu ya Msingi aliyoeleza huyo bosi,huwezi kuunda kikosi chenye wachezaji wapya ambacho hakikuwa Na pre season ukapata kila kitu kwa muda mfupi,wasubiri 4G tena
ReplyDeleteFalsafa ya yanga inajulikana, ina maana wakati mnaajiri kocha hamkucgunguza falsafa zake?
ReplyDelete