October 5, 2020

 


ETIENNE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania amesema kuwa wana imani ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 11 Uwanja wa Mkapa.


Leo Oktoba 5, timu ya Taifa ya Tanzania inatarajiwa kuingia kambini kuanza maandalizi ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ndayiragije amesema kuwa:"Tupo vizuri na imani ni kwamba tutafanya vizuri kwa kuwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi wana uzoefu mkubwa na wanajua kutimiza majukumu yao.

"Kabla ya kuwaita kwenye kikosi huwa ninakuwa na tabia ya kuwafuatilia kwa ukaribu hivyo tunaamini kwamba licha ya ushindani ambao tutakutana nao tutapata matokeo."


Miongoni mwa wachezaji ambao wameitwa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ni nyota Mbwana Samatta, Simon Msuva, Thomas Ulimwengu ambao wanakipiga soka la kulipwa nje ya Bongo.

Ndani ya Bongo wengine ni pamoja na Jonas Mkude, Fei Toto, David Kisu, Bakari Mwamnyeto na Ditram Nchimbi.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic