LEO Oktoba 6 Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) chini ya Rais Wallace Karia, limeingia makubaliano na Bia ya Serengeti Premium Lager na kusaini mkataba wa kuidhamini Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.
Makubaliano hayo yamefanyika mbele ya Waandishi wa Habari kwenye hafla fupi iliyofanyika Hotel ya Serena ambapo wamezindua pia na jezi za Timu ya Taifa ya Tanzania.
Uzinduzi wa jezi ulifanywa na Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas.
Mkataba huo ni wa miaka miatu wa kiasi cha shilingi bilioni 3 za Kitanzania.
Kwa sasa timu ya Taifa ya Tanzania ipo kambini ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Burundi utakaochezwa Oktoba 11, Uwanja wa Mkapa.
0 COMMENTS:
Post a Comment