WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo atakuwa mgeni rasmi wa mechi ya kirafiki ya kimataifa, ambapo Taifa Stars itacheza na timu ya Taifa ya Burundi.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi amethibitisha Majaliwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo ambao Stars, itakabiliana na Burundi.
Amesema mechi hiyo, imepangwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), itawahusisha wachezaji wa Stars wanaocheza ndani na nje,watakaoongozwa na nahodha Mbwana Samatta.
“Kwasababu hiyo, tunawasisitiza Watanzania, kujitokeza uwanjani Jumapili saa 10:00 jioni kwa wingi kuishangilia timu yetu, ambayo itatumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi nyingine za kimataifa za kimashindano zitakazoanza Novemba mwaka huu,” amesema Abbasi.
Stars iliweka kambi Oktoba 5 na kuanza kufanya mazoezi rasmi Oktoba 6 ambapo ni mchezaji mmoja aliondolewa kwenye ile orodha ya kwanza ambayo ilijumisha wachezaji 25.
Nyota huyo ni John Bocco wa Simba ambaye anasumbuliwa na majeraha aliyoyapata kwenye klabu yake ya Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment