October 11, 2020

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hauna mashaka na mechi zote ambazo zipo mbele zake kwenye ligi ikiwa ni pamoja na ule mchezo wao wa dabi dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Novemba 7, Uwanja wa Mkapa.

Mechi hiyo ilipaswa kuchezwa Oktoba 18 ila ilipelekwa mbele na Bodi ya Ligi Tanzania,(TBLB) kwa kile ilichoeleza kuwa ni kutokana na kuhofia vikwazo kwa usafiri wa wachezaji wa kimataifa wa timu hizo mbili walioitwa timu zao za taifa kutokana na uwepo wa vikwazo uliosababishwa na Janga la Corona.

Ofisa Muhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa hawana hofu na mchezo wao dhidi ya Simba wanaamini wakikutana nao lazima watawafunga bila matatizo.

“Kwanza tulikuwa tunawatamani kukutana nao hao Oktoba 18 kwa kuwa ni namba yetu ya bahati, bahati yao tarehe imepelekwa mbele mpaka Novemba 7, ila hiyo tarehe lazima itafika na tutafanya kweli.

“Ukitazama kwa harakaharaka kwa muda huu bado tupo kwenye ubora, hakuna ambacho wametuzidi kuanzia pointi na mechi za kushinda tupo sawa, na namna ambavyo tunakwenda tunazidi kuwa imara mpaka muda tutakaokutana nao muunganiko utakuwa bora zaidi,” amesema Nugaz.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo huku Simba ikiwa nafasi ya pili zote zina pointi 13 baada ya kucheza mechi tano, Simba imewazidi Yanga mabao ya kufunga ambapo wao wamefunga mabao 14 na Yanga imefunga mabao 7.

Mpaka kufika Novemba 7 kwa sasa kwenye mechi hiyo ya dabi  zimebaki siku 27.


4 COMMENTS:

  1. Kw nn tar 7/11/
    bora muda ungerudishwa nyma kwn 9/11/ Kna mech kat ya tunisia vs tanzania
    hawa tff wanakwama wp?
    mpk wanakeeeeeraaa

    ReplyDelete
  2. mpaka sasa hv bodi ya ligi ina maana hawajajua tarehe 9 kuna gemu kimataifa?

    ReplyDelete
  3. Tff wanatapatapa kwa ajiri ya kuibeba mikia Sasa ona wanavyozidi haribu,mikia bila tff no ubingwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic