October 6, 2020

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa hesabu kubwa ni kufanya maandalizi ya kikosi hicho kwa ajili ya mechi zake zijazo ndani ya Ligi Kuu Bara ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.


Kwa sasa timu zote Bongo zipo kwenye mapumziko ya muda ambayo yametokana na kuwepo kwa mechi za kirafiki zilizopo kwenye kalenda ya Fifa na Tanzania pia ina kibarua cha kumenyana na Burundi, Oktoba 11 Uwanja wa Mkapa.


Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kikubwa kilichopo kwa sasa ndani ya klabu hiyo ni kuendelea na maandalizi ili kukiweka kikosi tayari kwa ushindani.

"Tunajua kwamba kwa sasa kuna mapumziko ambayo yametokana na Fifa, kilichobaki kwetu ni kuendelea kufanya maandalizi ili kupata kile ambacho tunakihitaji.


"Malengo yetu ni kuendelea kupata matokeo chanya kwenye mechi zetu ambazo tutacheza ndani ya uwanja na hilo linawezekana kwa sababu tuna kikosi kizuri ambacho kimeshaanza kuleta muunganiko mzuri," amesema.


Zimebaki siku 12 kabla ya dabi itakayowakutanisha Yanga na Simba, Uwanja wa Mkapa, Oktoba 18 ambapo Yanga watakuwa wenyeji wa mchezo huo.


3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic