October 27, 2020



KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kimeendela kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United.


Mchezo huo ambao utakuwa ni wa nane kwa Yanga unatarajiwa kuchezwa Oktoba 30, Uwanja wa Kirumba.


Yanga inakutana na Biashara United ambayo imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania huku wao wakitoka kushinda mabao 2-1 dhidi ya KMC, Uwanja wa CCM Kirumba.


Kipa wao namba moja kwa sasa ndani ya Yanga ni Metacha Mnata ambaye amekaa langoni kwenye mechi sita kati ya saba akiwa amekusanya jumla ya clean sheet tano amefungwa bao moja na Hassan Kabunda wa KMC wakati Yanga ikishinda mabao 2-1.

Kaze amesema kuwa wanatambua wapo na ziara ya kikazi kanda ya ziwa lakini watapambana kupata pointi tatu kwenye kila mchezo ambao watacheza.


"Tupo na kazi kubwa ndani ya ligi, hapa imani yetu ni kwamba tutafikia malengo ambayo tumejiwekea taratibu kwani wachezaji wanajituma na wanafanya kazi kwa juhudi.


"Kilichobaki ni kuendelea kutoa sapoti kwa mashabiki katika mechi zetu ambazo tutacheza kwani uwepo wao mashabiki ndani ya uwanja unaongeza nguvu kwa wachezaji," amesema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic