ANTONIO Nugaz, Ofisa Uhamasishaji ndani ya Klabu ya Yanga ambaye leo Oktoba 10 ni kumbukizi yake ya kuletwa duniani, amesema kuwa sababu kubwa ya klabu hiyo kucheza mechi za kirafiki ni kutengeneza muunganiko mzuri.
Jana, Oktoba 9, Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki na Klabu ya Mwadui uliochezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.
Mchezo huo Yanga ilishinda bao 1-0 lililopachikwa kmiani na Michael Sarpong dakika ya 81 baada ya mabeki wa Mwadui na kipa kujichanganya kwenye kuokoa mpira huo.
Nugaz amesema:-" Kwa sasa tunahitaji kutengeneza kikosi makini ambacho kitakuwa kina uwezo wa kutoa burudani kwa mashabiki na kupata matokoe ya kupendeza ndani ya uwanja.
"Tunaijenga Yanga bora na yenye umakini kwa umakini mkubwa kupitia mechi za kirafiki hivyo mashabiki katika hili wasiwe na mashaka tupo imara.
"Ili kutengeneza mpatano wa timu kati ya wachezaji wakiwa uwanjani kwa kadri ambavyo wanacheza mechi za kirafiki zinaongeza muunganiko wa timu, ninawaomba mashabiki wazidi kutuunga mkono tunaamini tutakuwa imara," amesema.
Miongoni mwa mechi ambazo Yanga ilicheza Uwanja wa Azam Complex ilikuwa ni dhidi ya KMKM na Mlandege za Zanzibar na zote ilishinda kwa mabao 2-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment