October 10, 2020


Anaandika Saleh Jembe kwenda kwa Haji Manara namna hii:-

HAJI Manara umekuwa kivutio kwa vijana wengi kutamani kuwa wasemaji wa klabu, kazi ambayo miaka minne tu nyuma, hakuna aliyetamani kuifanya.


Ubunifu wako, uthubutu bila ya woga umefanya uibadilishe nafasi hiyo kutoka kuonekana ni ya watu wazima tu na sasa vijana wanaona ni kazi ya heshima na ufahari kuifanya.

Wasemaji wengi wametamani kufikia ulipo au kukupita na hii ni NEMBO YA MAFANIKIO.

Hakuna msemaji hata mmoja Afrika hii ameweza kutengeneza au kuichagiza misemo kadha wa kadha na sasa imekuwa misemo ya mpira ambayo imekuwa burudani, furaha na faraja ya mashabiki wa klabu yako ya Simba.

Umeanzisha kampeni kadha wa kadha, ukiwachambua na kuwadadavua wachezaji wa Simba na uwezo walionao kuwapa nguvu ya ushawishi Wanasimba wafike pale kwa MKAPA.

Nimeona NIKUSHAURI kwamba wakati mwingine kupuuzia KUNAEPUSHA mengi sana. Huwezi kujibu kila kitu na bahati mbaya sana, kila UNAPOFANYA MAZURI na kutengeneza UKUBWA, chuki huongezeka.

Kwa Tanzania, ukitaka upendwe sana ni kujipa stress. Ushauri wangu kwako, NYAMAZA TENA NYAMAZA SANA.

Najua wewe ni MZARAMO na mtani wangu, ulimi saa zote mdomo UNAWASHA...Lakini kunywa maji na UNYAMAZE.

7 COMMENTS:

  1. Kweli ukila nyama ya Binadamu nasikia uachi je na wewe Salehe u friends of Simba utaacha lini? Wewe Jerry Muro kawa msemaji Yanga mpaka Mkuu wa Wilaya asi wainspire watu ?wamwige matusi mdomoni?Hayo Ni mapenzi yako na Simba .

    ReplyDelete
  2. Muro Hana lakuiga maana yeye alikuwa anatukana mpaka kufikia hatua ya kuingiza ukabila mpirani nakuonywa na watu wazima. Hii siyo nchi ya ukabila site Ni Ndugu watanzania wenye furaha.

    ReplyDelete
  3. Saleh na Haji wote kitu kimoja, ndio maana muda mwingi wanatafuta kasoro za Yanga,
    Kama kweli ni mkweli angi sifu hata jambo moja la Jerry Muro lkn kwasababu lengo ni kuipaka matope Yanga, siku zote ameamua kuwaponda Yanga, lkn kwa bahati mbaya Hana madhara

    ReplyDelete
  4. Penye ukweli sema ukweli, utopolo huyo muro wao hakuwa na nidhamu mpaka kufungiwa na tff kwasababu ya matusi.

    ReplyDelete
  5. Tangia nianze kusoma ujumbe wako leo ndo naona weledi wako unaelekea kufika mwisho

    ReplyDelete
    Replies
    1. Et kwa mfano ueledi wa Saleh ukafika mwisho wewe utaathirika na nn na kama hautaathirika basi fanya yako maana huko uliko mengi uyafanyayo hayaridhishi wote unaoishi nao

      Delete
  6. Salehe mdanganye haji manara,Hana lolote muda mwingi anaisemea yanga,msemaji was club asemee timu iliyo mwajiri.mropokaji TU hana lolote.ikitokea unafahamu habari ya familia ya jirani kuliko yako ,basi yako itakushinda au utaikosa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic