KIKOSI cha Azam FC kimeendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya KMC utakaochezwa Uwanja wa Uhuru, Novemba 21 Uwanja wa Uhuru.
Azam FC ni vinara wa Ligi Kuu Bara, baada ya kucheza mechi 10 kwa msimu wa 2020/21.
Imejikusanyia jumla ya pointi 25 kibindoni na inafuatiwa na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 24 huku nafasi ya tatu ikiwa mikononi mwa Simba yenye pointi 20 zote zimecheza mechi 10.
Azam chini ya Aristica Cioaba imefanikiwa kufunga jumla ya mabao 18 na kinara wa utupiaji ni Prince Dube mwenye mabao sita na pasi nne za mabao.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wachezaji wanatambua kazi yao ni kusaka ushindi ndani ya uwanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment