November 17, 2020



 ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Novemba 21, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Ihefu ipo nafasi ya 18 kwenye msimamo ikiwa na pointi 5 inakutana na Polisi Tanzania iliyo nafasi ya saba na pointi 15 zote zikiwa zimecheza jumla ya mechi 10.


Uimara wa Polisi Tanzania ni kwenye safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Marcel Kaheza ikiwa imefunga mabao tisa inakutana na safu ya Ihefu inayoongozwa na Omary Mponda ikiwa imefunga mabao matatu.


Akizungumza na Saleh Jembe, Katwila ambaye aliibuka ndani ya Ihefu akichukua mikoba ya Maka Mwalisi aliyefutwa kazi Oktoba 6 amesema kuwa kila kitu kipo sawa.


"Maandalizi kwetu ni mazuri na kila kitu kipo sawa kwa sasa, wachezaji wana morali kubwa na wanahitaji kupata matokeo.


"Kupoteza mchezo wetu uliopita ni darasa kwetu tuna amini kwamba tutapata matokeo kwenye mechi zetu zijazo," amesema Katwila.


Mchezo wake wa kwanza kukaa benchi alishuhudia timu yake ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC Uwanja wa Sokoine na mchezo wake wa mwisho kabla ya ligi kusimama ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic