November 21, 2020


 JUMA Kaseja, nahodha wa Klabu ya  KMC leo Novemba 21 ameongoza kikosi chake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Azam FC ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 10 imepoteza mchezo wake wa pili leo na ule wa kwanza ilikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo ilifungwa pia bao 1-0 na kufanya ipoteza pointi sita kwa kufungwa huku ikiwa imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania.

Bao pekee la KMC lilifungwa na Relliats Lusajo mshambuliaji wa zamani wa Namungo dakika ya 57 na kufanya Azam FC wakwamwe kwa mara ya kwanza wakiwa Dar kwa kuwa ule mchezo wa kwanza walipoteza wakiwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Wakati Azam FC ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru,JKT Tanzania ikiwa nyumbani, Uwanja wa Jamhuri Dodoma imefungwa mabao 2-0 dhidi ya Gwambina.


Mabao ya Gwambina yamefungwa na Paul Nonga dakika ya 84 likiwa ni bao lake la kwanza ndani ya ligi kwa msimu huu wa 2020/21 na Meshack Abraham dakika ya 72 ambaye anafikisha bao lake la tano.

3 COMMENTS:

  1. Ila tu Lusajo na Adam Adam,na Nchimbi. Lusajo ana rekodi nzuri zaidi ya kufunga magoli anapoachwa kwenye kikosi cha Taifa stars hasa mara hii Samata aliumia kidogo inaleta ukakasi. Lusajo ana kimo kizuri mwili wenye nguvu ni dhahiri ni moja ya fowadi potential zaidi kwenye VPL na anaepaswa kuwepo Taifa stars japo akae Benchi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakubaliana nawe mkuu, labda haitwi/haonekani kwa sababu hachezei yanga, simba au azam. Pengine ataonekana

      Delete
  2. Walisema wanajambo Lao mbele ya KMC

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic